Malezi kwa Watoto wenye Ulemavu
Watoto wote, wakiwemo wale wenye ulemavu, wanahitaji mapenzi, heshima, malezi na muda.
1. Mlinde mtoto wako.
Weka nambari za dharura mahali unapoweza kuona kwa urahisi, kama juu ya jokofu 2. Kuwa msaidizi, mhurumie na kumpenda.
Mtoto wako anaweza kukosa usaidizi aliozoea, na hili linaweza kusababisha changamoto zaidi kama vile ongezeko la mfadhaiko, wasiwasi na hofu Tumia usaidizi wa kimwili na kimazungumzo kumfanya ahisi kuwa anakubalika na kupendwa Ishara nzuri za lugha na maneno huleta tofauti kubwa!
3. Wasiliana na mtoto wako.
Nyenyekea kwa kiwango cha mtoto wako unapowasiliana naye Mtazame na udumishe nia njema Mpe muda wa kuzungumza Mchunguze, msikize na umhakikishie kuwa unamwelewa
4. Mpongeze kwa mazuri.
Himiza uwezo na udhaifu wa mtoto wako kwa kumsifu na kutaja uwezo badala ya udhaifu Msaidie mtoto ikiwa tu anahitaji usaidizi. Usaidizi wa kupita kiasi humnyima fursa ya kujitegemea na anaweza kuhisi kuwa anatawaliwa
5. Omba usaidizi panapowezekana.
Shiriki mzigo na wanafamilia wengine Huko pekeyako! Ungana na watu wanaoelewa hali yako. Shiriki changamoto NA ufanisi wako Ni jambo la kawaida kuhisi mfadhaiko, hofu na kuwa na woga kwa wakati huu Jihurumie na upumzike unapohitaji!
6. Imarisha ratiba.
Ratiba huwafanya watoto kujihisi salama. Unda ratiba ya kila siku yenye shughuli anazofahamu mtoto wako na ujumuishe baadhi ya shughuli anazopenda Msaidie mtoto wako kutangamana na marafiki na wanafamilia kila siku kupitia chati za simu, kuandika kadi na kuchora picha Mpe mtoto wako chaguo mbalimbali ili aweze kuona kuwa ana udhibiti. Jambo hili linaongeza pia staha Tumia lugha inayoeleweka kwa urahisi na maagizo wazi na mawasiliano yasiyo ya mazungumzo kwa watoto wanaoyahitaji (kwa mfano: ishara, picha, vielelezo)