Kuwa na Furaha Nyumbani
Hapa kuna maoni ya vitu unavoweza fanya nyumbani ambazo zinahitaji vifaa vichache sana na ambazo zitafanya wakati wa nyumbani kuwa wa kufurahisha zaidi!

Hadithi katika Picha
- Fikiria hadithi unayofurahi kusikia au kuhadithia. Inaweza kuwa hadithi ya kweli, hadithi ya jadi, au hadithi unayotengeneza.
- Fikiria mandhari sita muhimu katika hadithi, pamoja na mwanzo na mwisho.
- Kunja karatasi katika mraba sita. Chora mandhari hizo sita muhimu kwenye masanduku.

Tafuta Ushairi
- Tumia siku kusikiliza vitu watu walio karibu na wewe wanasema. Andika maneno, misemo au sentensi unazosikia.
- Unda shairi kwa kuweka maneno, misemo au sentensi pamoja kwa mpangilio wowote unaopenda.

Kopo la Furaha
- Pata ujumbe chanya juu wa maisha na furaha kutoka kwa vitabu ambavyo umevisoma, vijana au watu wazima katika jamii. Ongeza maoni yako mwenyewe ya ubunifu kwa ujumbe chanya.
- Andika kila ujumbe kwenye karatasi ndogo na uweke kwenye kopo.
- Kila asubuhi vuta nukuu moja kutoka kwenye kopo na ujisomee mwenyewe au wengine

Kusanya tena Mosaiki
- Tafuta majarida na magazeti ya zamani, mifuko ya plastiki ya rangi tofauti, au chakavu cha kitambaa.
- Kata katika miraba midogo, angalau 1cm/1cm.
- Tengeneza picha kwa kugundisha miraba kwenye kipande cha karatasi

Fikiria Mahali Bora
- Chagua mahali katika jamii yako.
- Fikiria nini kingepafanya pawe mahali bora kwa vijana.
- Chora picha kuonyesha maono yako.

Fikiria Uvumbuzi
- Fikiria juu ya shida unayokumbana nayo kila siku. Inaweza kuwa shida kubwa au shida ndogo.
- Fikiria uvumbuzi ambao ungefanya shida kuwa bora au kuisuluhisha.
- Chora mchoro wa uvumbuzi uliyowaza. Andika maelezo ili watu wengine waweze kuelewa jinsi ingefanya kazi.

Jicho la Ndege na Jicho la Mdudu
- Fikiria mahali katika jamii yako panavyoonekana kupitia macho ya ndege anayeruka juu au ameketi juu ya mti. Chora picha ya kile angekiona.
- Fikiria mahali sawa kutoka kwa mtazamo wa mchwa au mbawakawa amesimama ardhini. Chora picha ya kile angeona.

Picha ya Fremu
- Tafuta vijiwe, chakavu ya karatasi au plastiki, gundi, na vipande vikubwa vya mstatili vya karatasi au gazeti.
- Gundisha vijiwe, chakavu au karatasi au plastiki karibu na mpaka wa vipande vikubwa vya mstatili wa karatasi. Wacha ikauke.
- Kata katikati ya karatasi na itumie kama muafaka wa picha