iogt vectors 2_what you ca do an observe new.png

Kipi unaweza kufanya na kutambua kwa watoto waliozaliwa?

Tazama machoni pa mtoto wako

UNACHOWEZA KUFANYA NA KUTAMBUA

  • Toa njia ambazo mtoto wako anaona, sikia, sogeza mikono na miguu kwa uhuru, kukugusa wewe. Mguso wa mwili ni kitu kizuri pia na kinaweza fanyika kila wakati.

Unapaswa kuona mikono na miguu ya mtoto wako ikiwa imetengana vizuri. Taratibu mtoto wako hujifunza jinsi ya kujiongoza mjongeo wake.

  • Tazama macho ya mtoto wako, na utabasamu pale mtoto wako anapotabasamu kwa kumuangalia usoni mwake.

Unapaswa kumuona mtoto wako akitoa jibu chanya kupitia uso wake, mjongeo na hisia zake. Mtoto wako huanza kujifunza kuwasiliana na utamuona jinsi anavyoweza kukujibu hata kabla ya kuzaliwa.

  • Tungumza na mtoto wako kwa kutumia sauti ya kuimba, na “Sauti ya mtoto”. Baba pamoja na mama wanapaswa kuzungumza na mtoto aliezaliwa.

Utafahamu kwamba anauwezo wa kusikia na karibuni ataanza kukariri na kufuatisha maneno yako.

  • Unaweza badili kwa taratibu sauti yako kwa polepole au haraka, juu au chini, kimya au kwa sauti.

Unapaswa kutambua majibu ya uso wa mtoto wako na mwili na kufahamu kwamba anashirikiana na wewe.

  • Weka mtoto kwenye tumbo lake. Gongesha kengele mbele yake na nyanyua kengele juu kidogo ili kuweza kumsihi anyanyue kichwa na mabega kuona ikisogea.

Kufanya hivyo itamsaidia mtoto kufuata kengele kwa macho, na zoezi katika kunyanyua kichwa na mabega. Wakati huo, atasikia sauti ya kengele ikilia.

  • Bembeleza, na mshikilie mtoto wako vizuri.

Utaona mtoto wako akijifariji na kuwa na furaha kushikiliwa na kukumbatiwa

  • Fanya ukaribu wa kimwili na mtoto wako kila muda

Unapaswa kumfanya mtoto kuwa salama na mtulivu kama vile anavyojihisi

Iliyotangulia Ifuatayo