Kwa nini ni muhimu kucheza na kujichanganya na mtoto?
Uzoefu mzuri wa mapema unasaidia ubongo wa mtoto kukua vizuri
Watoto wanakuwa wadadisi tangu pale wanapozaliwa. Wanataka kujifunza na kuelewa dunia ya kwao. Mwanzoni mwa umri wa miaka mitano ya maisha pia hata kabla ya miezi mitatu, ubongo wa watoto unakua kwa kasi Zaidi ya mida mwingine wowote. Uzoefu wa mapema wa watoto unapelekea jinsi gani ya kukua kwa ubongo wao na mafunzo ya mapema yana andaa ngazi ya mafanikio shuleni. Hivyo, uzoefu mzuri wa mapema unasaidia ubongo wa mtoto kukua vizuri. Kadri ubongo unapofanya kazi, ndivyo uwezo wa kufanya unaimarika. Wakati watoto wanapocheza ubongo wao hufanya sana kazi.
Uchezaji huja kwa kawaida kwa watoto na ndivyo wanavyojifunza. Fikiria kuhusu mtoto anaeanza kucheza mchezo wa kuficha uso pamoja na wewe wakati unapovuta shati lake kichwani. Au mtoto anaeanza kujifunza kutembea au mtoto mwenye umri wa miaka miwili anaefuatisha jinsi gani unavielezea vitu vinavyomzunguka. Mchezo umezajawa na nafasi nyingi kwa watoto kujifunza na kuunda ustadi mpya. Wakati watoto wanacheza, hutumia milango yao yote ya fahamu (Kusikia, kuona, kuonja, kugusa, kunusa na kusogea) kukusanya taarifa kuhusu dunia yao. Wanapangilana na kurudia kupangilia taarifa hii katika taswira yao ya kwanza, nyengine nay a dunia yao.
**Kupitia muunganiko mzuri na kujali, ucheshi na michezo, watoto watakua na ustadi mpya wa kuongea na kufikiri, kusogea na kufanya, kuhisi na kujifunza kuhusu wao wenyewe, na kujiweka pamoja na wengine.