iogt vectors 3_comforting time 6-9 baby.png

Wakati wa faraja kwa ajili ya watoto wa miezi 6-9!

Muache mtoto wako achunguze

UNACHOWEZA KUFANYA NA KUCHUNGUZA

  • Toa fursa kwa mtoto wako kutumia vitu safi na salama ya mifumo na maumbo tofauti.

  • Utaona akijaribu kupitisha vitu mkono kwa mkono na watu wengine, kuviangusha na kutazama wapi vimedondoka, sauti gani vinatoa, au kama mtu ataviokota.

  • Ita jina la mtoto wako kadri iwezekanavyo.

  • Unapaswa kuona mabadiliko ya muonekano wa mtoto wako, ambayo huonyesha anavyoitikia wito wako.

  • Wakati unakaa na kikundi kidogo cha watoto, watoto wachanga na watoto wadogo, unaweza pia kuchagua jina la mtu na kuimba kidogo kwa kutumia jina mtoto.

  • Mtoto wako polepole atakariri jina lake na kutambua mkiwa mnamzungumzia.

  • Ning’iniza picha mbalimbali katika chumba watoto 'kwa ajili ya yeye kuangalia. Unaweza kuning’iniza pete ya shanga na vitu rangi, ambavyo vinaweza kuwekwa juu ya kitanda ya mtoto au kuning’inia mbali na ukaribu wa mtoto.

  • Angalia vitabu vya picha na mtoto wako au watoto kadhaa kwa pamoja na uwaulize maswali rahisi kuhusu picha kuwasaidia kutumia au kuwaonyesha uelewa wa maneno.

  • Mtoto wako ataonyesha nia kwa kufuata picha kwa macho yake. Taratibu ataanza kujaribu kukariri.

  • Jibu sauti ya mtoto wako na nia yake.

  • Utagundua ongezeko la mtoto wako kujiamini na kujithamini.

  • Kata au chora kwa ukubwa, picha rahisi ya vitu vitavyomvutia mtoto. Bandika kwenye karatasi nzito. Toboa mashimo matatu katika upande wa kila ukurasa. Ziweke kwa pamoja kurasa tatu au nne. Weka vitabu kadhaa katika kikapu. Muache mtoto achague kitabu. Wakati mtoto anaangalia vitabu, msaidie kufungua kurasa na kuzungumza kuhusu picha.

  • Kukumbuka vitu anavyoviona na kusikia.

  • Weka kikaragosi kwenye mkono wako na fanya kizungumze na mtoto. Tumia sauti mbalimbali ili kufanya kikaragosi kifanye maongezi. Kifanye kikaragosi kijielezee kwa mtoto kuhusu chenyewe.

  • Utaona furaha ya mtoto wako na umakini vikiongezeka.

Iliyotangulia