Kucheza na mawasiliano na watoto mwezi 6-9
Watoto ni wanasayansi wadogo
JE, WAJUA?
-
Watoto hujaribu athari za mahusiano ya kawaida.
-
Watoto hujaribu jinsi gani vitu huanguka, jinsi ya kupiga kelele, upinzani wa mikono na miguu kwa kutumia nguvu.
-
Watoto hufurahia kupiga kelele au kugongagonga kikombe na vitu vingine. Hii inaweza kuwavunja moyo wazazi mama na baba lakini ni muhimu kuwa na subira wakati mtoto anajifunza kwa kuvichezea.
-
Hata kabla watoto kusema maneno, wao hujifunza kutokana na kile kilichosemwa kwao, na wanaweza kuelewa mengi.
-
Watoto hufahamu wakati watu wanaonyesha hasira kwao, na inaweza kuwakasirisha.
-
Watoto hunakali sauti na matendo ya wengine.
-
Watoto hupenda watu wengine kuikubali sauti yao na kuonyesha nia ya mambo mapya wanayoyagundua.
-
Mtoto anaweza kutambua jina lake kabla hajaweza kulisema. Kusikia jina lake humsaidia mtoto kujua kwamba yeye ni mtu maalum katika familia.