iogt vectors 3_useful tips for 6-9 bby.png

Dondoo muhimu kwa ajili ya watoto wa miezi 6 hadi 9.

Mazingira ya watoto yanachangia

DONDOO NA MIDOLI AMBAYO UNAWEZA KUTUMIA KWA AJILI YA WATOTO WA MIEZI 6 HADI 9.

  • Wakati kuuliza swali toa muda wa kutosha kwa ajili ya jibu. Hesabu mpaka 10 katika akili yako. Kisha kama hakuna jibu, ujibu swali mwenyewe. Jaribu swali rahisi wakati mwingine.

  • Hakikisha mazingira ya mtoto nyumbani ni safi na salama kuhimili vitu vinavyodondoka.

  • Sema jina la mtoto wako kadri uwezavyo. Yeye ataangalia kuona ni nani anamwita na atajaribu kuwasiliana na mtu huyo ambaye kwa anamwita.

  • Kamwe usiseme kwa sauti kubwa au kuimba kwa sauti kubwa pia kwa kuwa hii inaweza kuogopesha watoto.

  • Tabasamu kadri iwezekanavyo na umpatie mtoto wako faraja na uaminifu.

  • Vitu safi, salama, na vya rangi kutoka nyumbani, kama vile kijiko cha mbao au bakuli ya plastiki, inaweza kupewa kwa mtoto aguse.

  • Vitabu vya picha ni rahisi kutengeneza na ni vzuri sana kwa ajili ya watoto kuendeleza udadisi na kujifunza mambo mapya.

  • Vikaragosi vya mkono na wanasesere wa pamba: Fuatilizia kwa kalamu na kupanua muundo juu ya kitambaa. Kata vipande viwili vya mfano. Kwenye kipande moja, chora uso na kalamu ya wino au tumia vifungo au mbegu kwa ajili ya macho (hakikisha vipande vyote vimeungwa kwa usalama kwenye kikaragosi). Shonea vipande viwili pamoja, na kuacha chini pakiwa wazi, ili uweze kuingiza mkono wako.

  • Mafumbo yanaweza kusaidia watoto kujifunza jinsi maumbo, aina na rangi yanahusiana. Kutengeneza fumbo, gundisha picha kwenye ubao, mbao, au vifaa vingine vya aina hiyo, na ukate vipande kwa msumeno au mkasi.

Iliyotangulia Ifuatayo