iogt vectors_play and comm 9-12.png

Kucheza na kuwasiliana na watoto wa miezi 9 hadi 12

Kujichanganya na midoli

JE WAJUA?

  • Watoto wachanga hupenda kuichanganya na wazazi na walezi wao wengine. Watoto wanaweza kuwa na hofu juu ya kutokumwona mlezi waliemzoea.

  • Unaweza kumsaidia mtoto wako kujisikia salama, kwa kuwajibika wakati yeye akilia au akiwa ana njaa, na kwa kumtuliza kwa uwepo wako na kumfanya asikie sauti yako.

  • Kucheza kunaendelea kuwa ni wakati wa watoto wachanga kuchunguza na kujifunza kuhusu wao wenyewe, watu walio karibu nao, na dunia.

  • Kwa watoto wachanga wanapogundua vidole vyao, wanaweza kupata hamasa ya kugusa vitu kama midoli.

  • Watoto wachanga hufurahia kucheza mchezo wa kujificha (kombolela). Wakati baba anapojificha nyuma ya mti, wao kucheka kama baba atazuka na kuonekana tena. Wanafurahia kujificha chini ya nguo na hucheka wakati baba "anapowaona" wao.

  • Japokuwa watoto bado hawawezi kuzungumza, wao huonyesha kwamba wanaelewa ndugu wanachosema.

  • Watoto wachanga husikia majina ya vitu, na hufurahia katika kujua vitu hivo ni nini. Wao kuanza kuunganisha vitu kwa majina yao, kama vile neno ndege kwa mnyama katika kitabu au kwa ndege katika mti, na neno pua puani mwao.

Iliyotangulia