Kucheza na watoto wa miezi 9 hadi 12!
Furahia kujifunza kwa michezo
UNACHOWEZA KUFANYA NA KUCHUNGUZA
- Cheza mchezo wa kuficha na kutafuta na mtoto wako uone kama yeye ataweza kuvipata vitu unavyovificha. Unaweza kuficha vitu chini ya nguo na kumuuliza: “Imeenda wapi?” “Bado ipo huko?” “Unaweza kuitafuta?”
Unapaswa kuona udadisi wa mtoto wako ukiongezeka kwa nia ya kujua nini kilichotokea kwa kitu hicho.
- Mwambie mtoto wako majina ya vitu na watu wewe ambavyo unamaanisha.
Yeye lazima atakuonyesha nia na mda si mrefu ataanza kujaribu kufanya uhusiano kati ya maneno na vitu au watu.
- Muonyeshe mtoto wako jinsi ya kusema mambo kwa mikono, kama vile "kwaheri".
Mtoto wako lazima mda si mrefu atajaribu kukuiga wewe na yeye atapunga kuashiria kuaga mwenyewe, na kufanya uhusiano kati ya harakati na sauti.
- Nyooshea kidole kwenye macho, pua na mdomo za mwanasesere. Baada ya kuonyooshea sehemu mwili wa kwenye mwanasesere, gusa sehemu hiyo kwenye mwili wako wewe mwenyewe na kwenye mwili wa mtoto. Chukua mkono wa mtoto na umfanye na yeye aguse macho, pua na mdomo wa mwanasesere wako, na ajiguse yeye mwenyewe. Angalia pua juu ya mwanasesere? Hii ni pua yangu na hiyo ni pua yako.
Unapaswa kuona udadisi wa mtoto ukiongezeka. Taratibu, mtoto ataweza kukariri na kutambua maneno haya tofauti na kufanya uhusiano na sehemu za mwili wake.