iogt vectors 3_useful tips for 9-12.png

Dondoo za muhimu kwa ajili ya watoto wa miezi 9 hadi 12!

Kucheza pamoja

DONDOO NA MIDOLI AMBAYO UNAWEZA KUTUMIA KWA AJILI YA WATOTO WA MIAKA MIEZI 9 HADI 12

  • Wanafamilia wanaweza kufurahia kuwafundisha watoto wachanga mambo mapya. Wao wanaweza kucheza michezo ya mikono pamoja, kama vile kupunga "kwaheri", na kupiga makofi kwa kufatisha mdundo wa muziki.

  • Mwambie mtoto wako ukiwa unaondoka na umhakikishie ya kwamba utarudi mda si mrefu.

  • Unaweza kumwachia kitu vizuri na salama kwa mtoto wako mchanga - kitu ambacho kitafanya akukumbuke na kitamuhakikishia ya kuwa unarudi.

  • Kuwaongezea watoto wachanga hali ya kujithamini na kujiamini, daima weka mfumo chanya kwa mchakato wa kujifunza kwa mtoto wako. Mara nyingi zaidi jaribu kusema "ndiyo", "nzuri", "vema", badala ya "hapana", "mbaya", "si nzuri".

  • Midoli kama vile mwanasesere, mpira, inaweza kutengenezwa kwa kutumia vifaa vya kurudiwa matumizi na vitambaa.

  • Vyombo vya muziki vinawezakutengenezwa kwa kutumia fimbo za mbao, maburu na mbegu, nk. Unaweza kutengeneza kengele, kayamba, tari na vyombo vingine kwa urahisi zaidi.

Iliyotangulia Ifuatayo