how much do u reported copy.png

Kujibu maombi ya picha

Tafakari vyema kabla ya kutuma picha!

Nilikutana na msichana/mvulana nikampenda na sasa ananiomba nimtumie picha yangu. Sina uhakika kama kufanya hivyo ni jambo jema…?

Zingatia kwamba utakapokuwa umemtumia mtu picha au video - ya aina yoyote ile – hutaweza tena kudhibiti jambo lolote litakalofanyiwa vitu hivyo. Picha au video vinaweza kusambaa kwa kasi ya ajabu katika intaneti.

Unaweza kumuamini huyo mtu lakini endapo kwa bahati mbaya uhusiano wenu ukivunjika , au mkigombana au kama simu yako itaibiwa , picha au video uliyotuma vinaweza kutumiwa kukubughudhi au kukufanyia mambo ya kukuumiza.

Ni vigumu sana kuondoa picha/video katika intaneti baada ya kusambazwa.

Usifanye jambo ambalo utajalijutia.

Kidokezo cha intaneti kinachofuata:

Iliyotangulia Ifuatayo