how much do u reported copy 6.png

Kupokea ujumbe wa kujishindia fedha?

Jifunza kugundua utapeli!

Nimepokea ujumbe kutoka kwa mtu fulani kuwa nimejishindia fedha au tuzo – napaswa nifanye nini?

● Kama unatumia intaneti upo uwezekano mkubwa kupata barua pepe au ujumbe wa maandishi ukikuambia kuwa umejishindia fedha au tuzo kama vile simu ya kiganjani au safari ya kwenda mapumzikoni.

●Au, wakati mwingine ujumbe wa aina hiyo unaweza ukawa ni wa kukuomba umsaidie mtu fulani kutunza fedha zake.

●Kwa kawaida wanaotuma ujumbe wa aina hiyo watakuomba uwapatie taarifa zako mbalimbali kama vile namba yako ya akaunti ya benki au ya kitambulisho.

●Ujumbe wa aina hiyo ni utapeli.

●Haiyumkiniki kujishindia kitu fulani bila kushiriki shindano lolote.

●Usibofye katika maungio ndani ya barua pepe za watu usiowajua.

●Usidhubutu kutoa nywila yako au taarifa zako nyingine binafsi (kama namba ya kitambulisho, anuani au taarifa za kibenki ) kwa watu usiowafahamu.

Mada inayofuata

Iliyotangulia